BINTI WA KAZI SEHEMU YA PILI

 


Siku zote baba alikua anawahi kuamka na maji anajitengea mwenyewe..siku moja moja alikua anatenga mama akiwahi amka.
Siku moja nikaamua kubahatisha...huku nikiombea baba awe wa kwanza kuamka....
Nakumbuka niliamka saa kumi na moja kamili nikawasha mkaa na kutenga maji ya kuoga(kumbuka baba alikua anaoga maji ya baridi asubuhi)
mimi nikaamua mtengea ya moto...
Baada ya maji kupata moto nikamuandalia bafuni...(nikayanyunyizia iriki ili yatoe harufu nzuri)
nikaingia chumbani kwangu.nikachukua simu yangu ambayo nilinunua kama wiki mbili zilizopita...nikatafuta namba ya baba kwenye orodha ya majina nikaipata...
Huku nikitetemeka maana sijawahi mtumia SMS hata siku moja....na nikahofu iwapo ataiona mama hiyo SMS...lakini nikamwandikia.....BABA MAJI YA KUOGA TAYARI...KARIBU!!!!
BONYEZA HAPO KUSHARE kama umeikubali tupate nguvu ya kuendelea mwanzo mwisho....


No comments

Powered by Blogger.