MUME WANGU : 12

 

Mwandishi : Ascar Mnyenyelwa
Basi wapendwa baba yusuph alinijibu vile nliishiwa poz ukiangalia kimario yupo tayari kunichangia bas skutaka kuonyesha kuwa nmepewa jibu baya kwa mme wangu ikabidi nimuage kwa mahaba "sawa mume wangu Usiku mwema". Nlivyokata simu kimario aliumia Sana akasema siamini Amina Kama n wewe ambae kipindi kile hata wanaume ulikua unawaogopa leo hii unanifanyia hivyo Aya bana ngoja nimpigie dereva akufate maana naona nalazimisha Sana nsije kuuliwa na mwanaume mwenzangu bure!!!
Dah moyoni upande mwingine nlihisi vibaya nliona Kama nmemdharau kupita kiasi alaf nliona Kama nimefanya utoto kingine nliona Kama Mimi n mjinga huenda kimario ningemtumia vizuri ningepewa chochote kwa ajili ya mama. Bas nkakaa kidogo dreva tax akawa amefika kimario akachukua pombe akanywa kwa uchungu akaniaga kwaheri. Bas na mm ckutaka kujishusha kwa kuomba msamaha ikabid niondoke zangu. Kwenye tax nkawa nafikiria tuu nlivyomuacha kwenye mataa kimario utadhan simjui akat alikua ni mchumba wangu tuliependana lkn nilijipa moyo kuwa mm n mke wa mtu haitakiwi kuzini🙆
Basi nkarejea nyumbani nkakuta mama amelala , dada akanifungulia akaanza kumuuliza mawili matatu nkamueleza kila kitu maana mm na dada n Kama mashoga tuu sikumficha kitu dada alinambia umemfanyia dharau kubwa Sana kuongea na simu na mwanaume mbele yake japo ni mchepuko tuu lkn wanaume hawapendagi dharau hizo , nkamwambia kimario alitaka kuniongezea pesa kwaajili ya mama ndo nkamfanyia dharau hiyo nkiamini baba yusuph atatuma , dada alinishangaa Sana akasema inamaana humjui vizuri mumeo au nkamwambia dada najuta Sana , dada akasema mwombe msamaha mkaka wa watu bas tukacheka kwa pamoja.
Dada alinambia mdogo wangu Kama unavyoona mama anatutegemea sisi kwaiyo tupambane afya yake irejee wewe sio mtoto tumia akili maana ukisema utegemee mumeo unaona kabisa tabia zake Hana uchungu kabisa na mama yetu kwaiyo sisi ndo inabidi tuamke Kutafuta pesa iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri tukifanya mchezo tutampoteza mama , Kisha akaondoka.
Nlifikiria Sana , nkasema Sina jinsi ngoja nimtafute kimario, bas nkampigia simu hakupokea kabisa nkasema ntamchek kesho labda anahasira na Mimi , kesho asubuh nkamtafuta akasema alilewa akapitiwa nkamwomba radhi akasema alishanisamehe tangu Jana 😁 moyoni nkasema huyu anasema kweli au anataka kulipiza kitu🙄 bas nkamwambia sawa nlikua nakusalimu , kimario akasema njoo bas nmekumic kweli 😋 nkamjibu Sina nauli bana akasema usijali ntakutumia we kajiandae !!!!!
#Tutaendelea

No comments

Powered by Blogger.