MUME WANGU 07

Mwandishi : Ascar Mnyenyelwa

#tunaendelea


Basi, Siku zikaenda mwanangu akafikisha 40 jina lake lilikua ni yusra. dada ikabidi arudi kwake baba yusuph akapata safari Tena ikabidi asafiri. 

Maisha yaliendelea ivyo nlilea kwa tabu maana Kuna wakat yule binti alikua anaenda kusalimia kwao kwaiyo nlipata tabu kulea watoto wawili wadogo lkn Mungu alinisaidia mpk wakaanza masomo wakafika la tano mwingine la nne sikuzaa Tena kwaiyo nkawa nakula matunda yao tuu wanansaidia kazi , nawatuma dukani yaani nliona furaha ya kuwazaa sikujutia kamwe. 

Siku moja baba yusra /Yusuph alivyokua safari nkapigiwa simu kuwa mama yangu anaumwa ikabidi nimueleze baba yusuph alisikitika Sana akasema kwaiyo inabidi usafiri uende au tumtumie nauli aje! Kwakweli nilimshangaa Sana maana kawaida yake akiskiaga upande wetu Kuna mgonjwa au Kuna msiba anaishiaga kunipa tuu pole bas lkn alilibeba hili Jambo Kama mama yeke vile ndo anaeumwa, bas nkamweleza kuwa ngoja niongee na dada, nkaongea na dada , dada akasema kwasababu Mimi sina nyumba kubwa Cha muhim baba yusuph atume nauli ili mama afikie kwa dada , bas nkamweleza baba yusuph akasema anapambana kabla jua halijazama atume pesa ya nauli, kwakweli nlishukuru Mungu huyu mwanaume alivyojirekebisha. 

Kweli haikufika jioni pesa ikatumwa na ya kula njiani na yakutolea juu😁 nkamtumia mama, mama nae hakuamini macho yake akakatiwa ticket akaja dar kwaajili ya matibabu. Basi nkakaa siku mbili nkampigia baba yusuph kuwa inabid niende kwa dada nkamsaidie kukaa na mama , watoto itabidi wabaki na day dada kwa ajili ya shule , baba yusuph akasema nenda , nenda mama 😁 nlicheka Sana kimoyo moyo, bas nkawaacha wanangu maana walikua wakubwa wakubwa nkaenda kwa dada. 

Mama alianza matibabu , afya yake ilikua mbaya lakini siku zilivyozidi kwenda alikua anapata hafueni Kama mnavyojua uzee . Siku moja nikiwa kwa dada nakumbuka nlitoka Mara moja kwenda dukani nkakutana na yule mchaga wangu alokua anataka kunichumbia nlishtuka Sana ye mwenyewe alinishangaa na kusema nimenenepa Sana na kunawiri🙊 tukasalimiana pale akawa ananimwagia sifa kuniuliza nimepotelea wapi nmenenepa nmenawiri, nkamwambia nliolewa akasema dah we mwanamke , nkamwambia ndo ivyo na nna watoto wawili , alisikitika Sana akasema kwaiyo uliona Mimi nsingeweza kukupa watoto? Nkainama tuu sikujibu kitu. 

Basi akanilaumu pale akasema tangu nlivyomkataa aliona ajikite kwenye biashara na kwa Sasa anamalizia ujenzi hataki kuoa mpk afanye maisha yake nkamwambia hongera , akaomba tubadilishane namba🤸

#tutaendelea


 

No comments

Powered by Blogger.