MUME WANGU 05


Mwandishi : Ascar Mnyenyelwa

#tunaendelea

Basi wapendwa maisha yangu yakawa ndo hayo mume kuniona mtoto Kama kuna wanaopitia changamoto Kama yangu wanaelewa mume akishakuona mtoto hata Kama kuna Jambo la maendeleo analishughulikia Kuna mda hakwambii anasubir likamilike labda ndo akueleze yaani ilikua kila sector lazima yeye aseme yaan Mimi kusimama Kama mama alikua anaona siwezi ilifika wakati mpaka nkifanya usafi au nkipika chakula anaanza kukikosoa yaani ilikua ndo maisha yetu baba yusuph alijibebea majukumu yote kwakweli nlikua sioni thamani yangu Kama mwanamke sijui nlikua namuonaje au sijui wanaume wa ivyo wanamaanishaga Nini.

Siku moja akiwa bado yupo nyumbani , yaani hajapata safari dada yangu alikua anaumwa Sana na binti yake wa Kaz hakuwepo ikabidi apige simu niende, kumueleza baba yusuph alinikatalia katu katu hataki niende, nlijiskia vibaya mno nkamwambia leo kwake kesho kwangu unavyonikatalia nsiende kuona wagonjwa Tena ndugu yangu unantengenezea uadui nami sinto saidiwa , mume wangu alikataa akasema mke wangu sitaki utoke kabisa wewe ni mzuri najua mumeo nnakisirani unaweza usirudi, moyoni nkasema kumbe anajijua anakisirani. Nkamwambia bas nenda wewe mwenyewe akasema akipata nafasi atakwenda.

Dada yangu aliendelea na matibabu alivyokaa sawa akatupigia simu akanichamba akaomba simu aongee na mme wangu nae akamsema haswaa tabia hii tuiache, mume wangu alivyokua hana haya maskini hakukaa kimya alitukanana na dada yangu kisa kuambiwa ukweli roho iliniuma mno wakawa wamejenga chili mtu na shemej yangu. Basi baba yusuph akapata safari Tena nakumbuka kipind hicho mwanangu alikua kafunga mwaka nkajikuta Tena nna ujauzito nlimtaarifu baba yusuph alishtuka Sana akasema inabidi niitoe nkamwambia siwez kutoa na Kama nkitoa nataka uwepo karibu yangu uniuguze mwenyewe maana ulishajibu vibaya ndugu zangu Nan wa kuniuguza japo binti tunae humu ndani lkn hawez kuniuguza swala la kipumbav Kama hili , baba yusuph kwa hasira akasema Basi Zaa. 

Nlijaribu kumshirikisha dada akasema usitoe utateseka wakiwa wadogo lkn wakikua utaenjoy bas nkaskiliza ushauri wa dada nkaanza kulea mimba ya pili. Basi siku zilivyokwenda mume akarejea akanikuta na tumbo la miez minne , maisha yakaendelea Mungu akanisaidia ikafika siku ya uchungu ambapo mimba ya pili sikwenda nyumbani nakumbuka siku iyo binti alitoka kidogo nkabaki na yusuph na baba yake , uchungu ulinianza baba yusuph kachanganyikiwa hana jinsi akampigia wifi hapatkani ndugu zake karibia wote siku iyo cjui ilikuaje hawakushika simu akawa Hana jinsi akapiga kwa dada yangu kuomba msaada!!!!!!!

#tutaendelea

No comments

Powered by Blogger.