MUME WANGU 04
Mwandishi : Ascar Mnyenyelwa
#Tunaendelea
Basi jamani maisha yangu yakawa ni hayo mme wangu akiwa safari bas Kaz zisifanyike nihakikishe simu imejaa chaj maana akipiga sipatkaniki kosa pia natakiwa nsiongee na mtu maana akipiga nnatumika kosa , akipiga sipokei napo kosa. Alikua akisafiri anakaa miez miwili mpk mitatu alaf anarejea nyumbani akishajerea nyumbani ndo angalau hata natupilia mbali simu licha ya mm kutokua karibu na simu akitokaga safari hua anapanda Sana kukagua simu yangu akikuta lolote asilolielewa atapiga simu kuuliza asichokielewa Kama n marafiki atampigia ajue nimejuana nae vipi.
Tisa kumi alikua akirudi simu yangu inakua yake kila ikiita yeye ndo anapokea Kwanza kma mtu anataka kuongea na Mimi anaanza kuongea nae Kwanza ndo na Mimi naongea kwakweli nlikua upande mwingine naona kero kubwa Sana maana Kuna vitu ambavyo n vyakifamilia unatamani ujiachie uongee au uchat na dada lkn nashindwa yaan alikua ananibana Sana japo upande mwingine nahisi Kama napendwa sana.
Siku moja alisafiri Kama kawaida yake baada ya wiki Tatu akarejea nyumbani kikawaida anarudigi na vitunguu vya kutosha nyanya , viazi , Michele, mafuta ya kula yaan mazagazaga yote alivyofika nyumbani nkamkaribisha vizuri kesho yake akaja dada yake kunisalimia , hiyo dada ake kila baba yusuph alisafiri dada ake anakujaga Sasa sijui hua anamtaarifu au vipi na akija Nampa vitu alivyoleta Kaka yake nae apate kidogo. Bas siku iyo alivyokuja tukapiga story tukala jioni wifi akawa ananiaga ili aondoke lakini kabla hajaondoka alinambia kuwa Leo haitaji chochote maana Kama n vitu bado anavyo naona aliona aibu , Basi muda ulivyofika wa yeye kuondoka ikabidi wifi amuite Kaka yake aje seblen amuage maana aliingia ndani Mara moja.
Basi baba yusuph akatoka kumuaga dada yake Mimi nami nkawa na muaga ba yusuph alinikata jicho akishangaa mbona sihangaiki kumfungashia mizigo alivyoona dada yake anataka afungue mlango aende akaanza kunichamba yule mwanaume , kwanini humpi dada vitu akale na wanae , oooh we mwanamke mchoyo Sana yaan yalimtoka maneno mengi Sana dada ake akamwambia sio vyema unavyofanya wewe unafamilia Kaka yangu kila siku ukisema ulete vitu ugawe kwetu unadhani familia yako itakula nn hata ivyo mm ndo mwenye makosa nlimwambia asinipe safari hii unavyogawa mavitu kwa ndugu wewe ulishawah kuletewa , maana unakuta ukija na vitu karibia nusu na robo vinaenda kwa ndugu nyie mnabakiwa na hiyo robo ukisafiri baada ya siku kadhaa vitu vyote vimeisha mnaanza kununua akat mkeo asingegawa angalau ungekuta bajet ingepungua ndani na maendeleo yangefanyika.
Kwakweli wifi yangu aliongea maneno makali na mazuri Sana hakupenda Kaka yake alivyonigombeza japo wakija ndugu zake wengine wanafurahigi wanavyopewa vitu na Kaka yao Tisa kumi anapenda kugawa kwa ndugu zake tuu. Hilo Jambo lilizidi kuniumiza kwakweli. Yaani kiufupi mume wangu alikua na gubu, maneno mengi, wivu mkali, pia alipenda kujiona mtoaji au mgawaji yaan Kuna wakat ata akirudi safari mgeni atakae kuja ndani Kama n ndugu ama rafiki kugawa elf kumi kumi kwa watoto kwake ni sawa ukizingatia hatuna hata kiwanja.
Ndoa hizi Kama hujakomaa kuyabeba Mambo inataka moyo unaweza Lia kila siku
#Tutaendelea
Leave a Comment