MUME WANGU 02

                           

                        MUME WANGU 02

Hatimae Mimi na mume wangu  tukawa rasmi Mr and Mrs tukaanza maisha rasmi katika nyumba ya kupanga ilikua ni mbali na kwa dada yangu japo ilikua ni hiyo hiyo dar. Kwakweli kwasababu nlikua sijazoea kulala na mwanaume nlikua ni mshamba haswa hata kufanya mapenz alikua akinibembeleza Sana maana anajua nlikua naogopa ukizingatia ye n mtu mzima. 

Ilifika wakati akawa ananambia umeamua kuolewa sharti uniskilize mumeo lkn naona hutaki kabisa au unataka kurudi kwenu , dah nliwaza nkaogopa kuwatia aibu wazazi ikabidi nimuambie kuwa ntajaribu japo naogopa pia naumia Sana. Akasema pole Sana ntafanya taratibu taratibu. 

Basi ikawa ni hivyo ndani ya wiki moja nkawa nmezoea mchezo nlivyofunga mwez nkajikuta period imekata sioni siku zangu nkamueleza mume wangu akafurahi Sana akasema mke wangu unamimba. Kwakweli nliogopa nliwaza tuu mtoto atatokaje maana nlijiona n mdogo lkn nkasema Kuna watu wanazaa umri mdogo kushinda mm nkajipa moyo . 

Mume wangu alikua ni wafuraha mda wote hasa alivyoona nna mimba alinijali Sana alikua na wivu Sana kiasi kwamba hakutaka niende hata dukani. Alikua akinunua mahitaji yote ndani ili nistoke nje hakutaka kabisa nisimame na mwanaume yoyote yaani alikua anawivu mpk kero. Akienda kazini aniache ndani na akirudi anikute ndani tuu. 

Siku zikaendelea kwenda mimba ikakua kubwa amani iliendelea japo kasoro yake ilikua ni ya wivu tuu yaan alikua akinikuta hata naongea nampangaji mwenzangu anaweza akamtukana matus yote alikua anataka nikae ndani tuu , sikumuelewa kwakweli na nlichukia tabia yake.

#itaendelea


No comments

Powered by Blogger.