MUME WANGU 01
MUME WANGU 01
Mwandishi : Ascar Mnyenyelwa
Karibuni Tena katika simulizi mpya ya #MumeWangu , Kama mnavyojua hizi simulizi ni za ukweli na zinagusa maisha ya watu mbalimbali Mimi ni kijumbe tuu naskiliza simulizi ya mtu au anaiandika Mimi naipitia upya kusahihisha alipokosea maandishi ili nikiwaletea kitu kiwe kinachosomeka vyema na kueleweka. Nazidi kuwaalika wale wenye story zao za ukweli walizozipitia katika maisha yao ambazo wangependa kutusimulia ili tuzidi kujifunza Mambo mengi zaidi. Nawaalika mfatilie simulizi hii mwanzo mpaka mwisho 🙏
#Tunaanza
Jina langu naitwa Amina kabira langu ni mrangi elimu yangu niliishia darasa la Saba huko kijijini baada ya hapo nikaenda dar es salaam kwa dada yangu ambae alishaolewa na kuzaa watoto watatu. Kiukweli tamaduni zetu zinapenda Sana mwanamke ujistiri uolewe hazijaweka kipaumbele Sana katika masomo pia hata Kama ni ndoa bas tunaoana ndugu kwa ndugu. Bas nlivyofika kwa dada , mama yangu alimsihi Sana dada anichunge nijitunze nsije tolewa bikra maana haitoleta heshima kwa mume ntakaeozeshwa.
Kwa kipindi hicho nlikua na miaka 17 naelekea 18 ambapo nliishi kwa dada tangu nmemaliza la 7 mpk nkafikisha iyo miaka 17 hapo ndipo ndugu waliona naelekea utuuzima na nnafaa kuolewa. Kabla ya Mambo ya ndoa Kuna kijana wa kichaga alinipenda Sana nlimueleza dada lkn dada alinambia nitulie ntatafutiwa mume siwez kuolewa mbali huko . Bas siku zikaenda , siku moja nkapewa taarifa kuwa ndoa yangu inakaribia . Nliuliza vipi kuhusu mwanaume mbona simjui , dada akasema atakuja utamuona ataleta barua na mahali kisha atakujaribu kuona Kama hujatumiwa na mwanaume yoyote akishajiridhisha ndipo tutaandaa tarehe ya ndoa mfunge ndoa.
Kwakweli nliwaza na kuomba Mungu mwanaume atakaekuja tuendane na awe na mapenz ya kweli maana hata ningekataa kwa Mila zetu ningejitia nuksi nsingeweza kuolewa Tena kwaiyo ilikua ni furaha mpk kwa familia. Basi siku ikafika Mambo yakaenda Kama ilivyopangwa nkaonana na uyo bwana nkatambulishwa kuwa ni mjomba wangu kwakweli naweza kusema ndio alikua mjomba wangu lkn sikuwah kuwa na mazoea nae pia alikua n mkubwa Sana kwangu kanizid Kama miaka 20 lakini kwasababu ni Mila zetu kuoana ndugu ikawa ni sawa tuu.
Kweli yule bwana alitest mitambo akaona sijafunguliwa😁 ndoa ikafungwa Mila na desturi zikafanyika za kuchinja mbuzi ishara ya kuondoa kuoneana aibu baina yangu mm na mjomba.
#tutaendelea
Leave a Comment