MUME WANGU 08


 Mwandishi : Ascar Mnyenyelwa

#Tunaendelea

Basi kimario akaniomba pale namba ikabidi nimpe lkn nkamwambia utakua ukinipigia utaongea Nini labda iwe salamu tuu maana mm nshaolewa, akasema dah Amina , kwaiyo huyo mume ndo hata kuongea na watu hataki hivi nlijua nyumba ntakayoijenga tutaishi wote , nkamwambia hapana kimario Mimi nshaolewa akasema okey mmejenga maeneo gani , nkamwambia bado tumepanga akasema sawa karibu kwangu Mimi bado sijaoa kwaiyo najua kabisa wewe huwez kunikaribisha kwako lkn Mimi bado ni rafiki yako siku yoyote unakaribishwa kwangu.

Basi nkacheka pale nkamwambia kimario punguza kuongea bana Mimi sio Amina wa zamani Mimi ni mama yusuph au mama Yusra , kimario akasema kwani kuzaa kitu gani bana u ajikuta umekuua kumbe ni kabinti ka 98 umekua nakuona kabisa , akaongea hivyo huku akinipiga begani kimasihara , nkamwambia shauri yako , akasema Aya bana bas tutawasiliana ebu nkachek mzigo wa dukani. 

Basi tukaagana pale , nkarudi zangu kwa dada sijakaa Sana kimario akapiga , nkapokea simu akasema bado unamuuguza mama jioni ya Leo naweza kukuona? Nkamwambia kimario najuta kuchukua namba zako hivi ningekua kwa mme wangu ndo unganipigia hivi , akasema aaahaaa bana umesahau ulinambia unamuuguza mama mpk apone ndo maana nkakupigia Amina , hivi Amina unaona upo sawa kuniacha mwenzio njia panda akat tulikua tunapendana wazaz tuu ndo walikataa nsikuoe ili uolewe na ndugu hawala Hana talaka bana . 

Kimario jamani alikua ni muongeaji mno ikabidi nimwambie nauguza bana Kwanza mama yangu tuu kaishiwa Ela ya supu alaf Mimi nihangaike huko na wewe , kimario akasema Amina unatoa sababu nyingi hutaki tuonane eeh nkamwambia si tulishaonana mchana akasema okey ntakutumia sasaivi Ela umnunulie supu mama mpk ya kesho ili usisumbuke , nkamwambia mpk kesho? Unamaana gani Mimi ntalala uko au akasema nakutumia nakutumia chap !!! Akakata simu 

#tutaendelea

No comments

Powered by Blogger.