MUME WANGU 06
Mwandishi : Ascar Mnyenyelwa
#tunaendelea
Basi ikabidi apige simu kwa dada , dada akapokea akauliza kulikoni leo amekumbukwa , baba yusuph akamwomba aje amsaidie , dada akasema ebu mpe niongee nae bas nkaongea nae akauliza simu ipo loud speaker nkasema hapana akasema mdogo wangu vipi Hali yako unajihisije nkamwambia ni uchungu tuu unakuja na kukata akasema Sasa huyo mumeo nataka tumfunze wewe sio uzazi wako wa Kwanza unaelewa Cha msingi jilize ili achanganyikiwe hata Kama uchungu umekata jilize haswa ili siku nyingine ajifunze Kama ushapaki vifaa vya kujifungulia mwambie akupeleke sisi tutakuja kukuona hospitali.
Basi nkamrudishia simu baba yusuph , dada akasema kuwa kabanwa Sana nakazi(alimwambia ba yusuph makusudi) baba yusuph akashikwa na uoga akamwambia Hali ya mdogo wako sio nzuri nakuomba Shem naomba tusameheane yote jmn haya Mambo ya kike mm siyawez dada akasema tatizo kazi zimebana huku Cha muhimu muwahishe hospitali baadae nkipata muda ntakuja, baba yusuph alichanganyikiwa Sana na Mimi nlikua ndo nazidisha kumtia presha makusudi. Basi akaniwahisha hospitali huku akimtafuta dada Mara kwa Mara akimuomba amtumie pesa hata apande boda boda ilimradi tuu dada aniwahi mimi. Dada alimwambia hana shida na pesa anaogopa kuomba ruksa atapoteza kazi yake. Basi tulivyofika hospitali nkamwambia baba yusuph nataka maji, alivyoenda nkampigia dada , dada akasema nakuonea uchungu mdogo wangu nshakuandalia chakula nakuja nacho akaulizia pia Hali yangu nkamwambia uchungu bado unakuja na kukata akasema mwambie baba yusuph arudi na mtoto Mimi nakuja .
Basi nkaletewa maji nkamwambia aondoke na mtoto mm niingie hodini kwakweli nlimuona baba yusuph kachanganyikiwa haswa na alijenga heshima kubwa kwa dada yangu alijuta alomfanyia dada kipind kile.
#tutaendelea
Leave a Comment