MUME WANGU 03

                                         MUME WANGU 03

Kabla ya kuendelea Kuna watu walikua wanashangaa mjomba kivipi kiukweli mm nliambiwa ni mjomba tuu naona n ndugu wa mbali maana uongo dhambi mm nlikua namskia tuu lkn mjue tuu n ndugu maana kabila letu n kawaida kuoana ndugu kwaiyo nlichaguliwa wa mbali lkn nliambiwa ni Kama mjomba vile nlivyoelekezwa na wakubwa zangu.

Basi tuendelee tulipoishia, Kama nlivyosema tabia yake ambayo ilikua n too much ni iyo ya wivu alikua anakauli Kali Sana endapo akinikuta naongea na mtu hasa wakiume. Bas siku zikasonga ikabidi nirudi kwetu kondoa kwaajili ya kujifungua. 

Alinipa pesa ya kutosha kwaajili ya matumizi huko Mungu akanisaidia nkajifungua pale pale nyumbani mtoto wa kiume ambalo alipewa jina la Yusuph bas nkawa natambulika rasmi Kama mama Yusuph. Baada ya kumaliza uzazi na kukandwa maji ikabidi nirejee kwangu dar es salama ambapo nlikuja na binti mmoja ambae ni ndugu wa baba Yusuph anamuita ba Yusuph mjomba alafu Mimi kwake ni Kama mtu na binamu , yaan kiufupi ndugu zake na baba Yusuph hawakua wakwe tuu Bali nlikua naundugu nao wa mbali nadhani naeleweka wapendwa. 

Basi nkarudi na yule binti ili anisaidie kazi kweli alikua anajitahidi tulikaa pamoja mwaka mzima akinisaidia kulea mtoto, mume wangu akapata kazi nyingine ya kusafiri na magari makubwa ya kwenda Zambia kwaiyo tukawa tunaishi sisi tuu. 

Hali ya mume wangu kusafiri ilijenga wivu kuongezeka yaani nilikua nakonda kwa kauli zake Kali pale ambapo yupo safari alaf anapiga simu sijapokea alikua akinitukana Sana alikua na maneno machafu mno hiyo kitu ilinifanya niumie Sana nikose amani nkaona nanyanyasika ukizingatia yule alonitaka mwanzo (mchaga) alikua akininyenyekea maana hata Kama ni wivu baba yusuph alizidisha 

#tutaendelea

 

No comments

Powered by Blogger.