MUME WANGU : 10

 

Mwandishi : Ascar Mnyenyelwa

#tunaendelea

Basi bwana kimario alinitoa out kweli kweli nlikula nkanywa na vinywaji kwakweli nilienjoy maana mume wangu hakuwahi nifanyia hivyo hata nlivyomzaa watoto hao wawili mume wangu alikua ananinanga Sana oooho umeharibika, oooho umekua na tumbo kubwa Mara sijipendi mbona zari anawatoto watano hajaaribika hivyo wewe viwili tuu lkn unaonekana Kama mama wa miaka arubaini , yaani nlikua Sina amani mpk alishawah kunambia kuwa kutokana na nlivyonenepa hata kuongozana na Mimi anaona aibu.

Lakini mume wangu baba yusuph ni mwanaume alokua anajali familia Hilo sikatai shida yake ndo iyo unafanywa Kama kuku yaani hayuko proud na Mimi hajivunii Mimi kabisa yaan kusema mke na mume eti tutoke Hilo haliwezekani anasema mpk mwili upungue lakini kwa kimario yaani alikua anajivunia Sana Mimi yaani alikua anapenda kuwa na muda na Mimi alaf aliniheshim Sana na hakuona kuwa nimeharibika maana alikua anapenda ubonge. 

Basi Tuachane na hayo tuendelee Sasa, kiukweli ile siku nilienjoy mno nkajiona Kama nimekua binti yaan zile kashfa za baba yusuph nliona za uongo maana nlijiona mtu mbele za watu , Basi mida ikawa imeenda nkamwambia kimario mda umeenda muite yule dereva anifate au nikapande tuu boda boda nirudi nyumbani , kimario akasema mbona unawahi hivyo subiri subiri bana wewe, nkamwambia usiku Sasa umeingia akasema okey Basi ngoja Kuna kitu nataka nkakifatilie Mara moja chap nkirudi ndo utaondoka , akaacha simu mezani akaenda. 

Nkakaa kidogo waiter akaja akanambia kimario anakuita anaomba umpelekee simu zake , nkamuuliza wapi? Akasema nifwate nkuonyeshe alipo , duuu nliogopa lkn nkasema ngoja nimpelekee fasta niende maana pale kulikua na watu ningemkatalia waiter au ningeonyesha kujibizana watu wangeniangalia kwaiyo nkaona aibu nkanyanyuka kumfata waiter, waiter akanipeleka mpaka alipo kimario , nlimkuta yupo kwenye chumba kilichoandaliwa vizuri maana pale palikua n bar na lodge nlishtuka nkasema Nini hiki🙄🙄

#tutaendelea


No comments

Powered by Blogger.