MUME WANGU 09

Mwandishi : Ascar Mnyenyelwa

#tunaendelea

Basi kimario hakukaa mda mrefu mesej ikaingia nimepokea sh elf 40 , mmh nlishangaa nkawaza ubahili wa wachaga mmh Basi akapiga nkamwambia Aya nimeipata akasema okey usisahau Kuna baadae mama. Nkamwambia ntakuja tuu tupige story akachaka akasema mbona unamashaka mama naelewa wewe ni mke wa mtu hata mm n rafiki yako utakuja tuu tupige story upate vinywaji angalau upunguze stress za kumuuguza mama. Basi nkamwambia sawa. 

Kweli jioni ikafika ikabidi nmdokeze dada , dada alinambia we ushakua mkubwa watoto wawili unajua baya na jema nkamwambia hata hivyo nmesahau kukukabidhi hii elf 40 akasema ya nn mdogo wangu nkamwambia kimario alituma kwa ajili ya mama , dada akacheka akasema usinambie nkamwambia ndo hivyo dada. 

Dada alijisemea tuu haya mdogo wangu akili ku mkichwa Kama mwaenda kupiga story Mara moja haya maana wewe n mtu mzima siwez kukuchunga lkn kua makini mumeo c unamjua na ukali wake nkamwambia yaani atanikata maskio , wote tukacheka kwa furaha . Basi jioni ikafika nkajiandaa zangu nlivaa tuu suluari na kiblauz Cha kubana pamoja na koti refu refu la kuchona kwa juu , kimario alikua akinipigia kuuliza Kama nshatoka nyumbani nkamwambia ndo najiandaa akasema sawa ukimaliza nishtue nitume tax , bas nlivyomaliza nkasema ngoja nimpigie Kwanza mme wangu nimjulie Hali, nlimpigia kweli akapokea akanambia anakaribia mpakani kwaiyo hatopatikana kwa kawaida mpk watsap nkamwambia sawa bas tukaongea ongea pale tukamalizana na mume.

Kidogo akapiga kimario kujua kama nmemaliza nkamwambia ndio akatuma tax ije kunichukua na kunipeleka mpaka alipo , tax ilinifikisha mpaka kwenye bar ilikua imechangamka upande mwingine imepoa kwaajili ya kupiga story nkamkuta kimario yupo upande wa palipopoa nkamwambia wewe na uongeaji wako ndo umeamua kukaa patulivu ivyo akasema si kwasabab tunapiga story 😁 bas nkaketi pale akanisifia nmependeza Sana nkamwambia Asante rafiki. Akanambia agiza unachotaka , kwakweli kimoyoni nlijiskia furaha maana mume wangu hakuwahi kunitoa out yaan licha ya kunitoa out alikua hawez hata kupngozana na Mimi mpk nkawa najihisi vibaya labda nilivyozaa nimezeeka au vipi lkn kimario alinifanya nijione bado nalipa maana alikua anaenjoy Sana kuwa na Mimi. Mume wangu alikua yupo radhi anunue mapochopocho alete ndani lkn sio Mimi kutoka nae . 

Ngoja nipige kinywaji Kwanza 

#Tutaendelea

 

No comments

Powered by Blogger.